4.45B imeleta tabasamu kwa wanafunzi wa kike Kilindi, Tanga

Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Februari 25, 2025 amezindua shule ya sekondari ya Wasichana mkoani Tanga iliyopo Wilayani Kilindi ambapo amependekeza iitwe jina la Mbunge wa zamani wa Kilindi Beatrice Shelukindo.

Shule hiyo imejengwa kwa thamani ya shilingi bilioni 4.45 ambapo kuna madarasa 12 ya kidato cha kwanza hadi cha nne, choo chenye matundu 16, jengo la utawala, bwalo/ukumbi wa mikutano, maabara 4 ambazo ni maabara ya Biologia, Fizikia, Kemia na Jografia.

Pia, kuna madarasa 10 kidato cha tano na sita, nyumba 8 za walimu, mabweni 12, nyumba ya nishati na zahanati yenye vifaa vya kisasa na wataalamu wa afya.

Baadhi ya wazazi wamempongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa shule hiyo kwamba imesaidia kuondoa changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu.