Miradi ya maendeleo Tanga yawaibui viongozi wa dini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Handeni katika mwendelezo wa Ziara yake ya siku saba ndani ya mkoa wa Tanga. 

Jengo hilo lina thamani ya Tshs. Bilioni 3.6 likiwa na vyumba 61 na Kumbi 03.

Wakizungumza baada ya uzinduzi huo, baadhi ya Viongozi wa Dini wamemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada anazozifanya za kuleta maendeleo katika nyanja mbalimbali ikiwemo huduma ya Maji Safi na Salama.