Timu nne za Ligi Kuu ya wanawake kushiriki Samia Women Cup 2025

Klabu za Simba, Yanga, JKT na Fountain Gate kwa upande wa wanawake zitashiriki mashindano ya Samia Women Cup 2025 yatakayofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid Jijini Arusha kuanzia Machi 4, 2025.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limethibitisha kupokea mualiko kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ukizialika timu hizo nne za nne za Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL) 2024/2025.

Timu zote zitawasili Arusha Jumapili Machi 2, 2025.

Mashindano hayo yanafanyika kwa mara ya kwanza katika wiki ya kuelekea kilele cha Siku ya Wanawake Duniani ambayo Kitaifa itafanyika jijini Arusha.

Michezo ya nusu fainali itachezwa Machi 4, 2025 na mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu na fainali itachezwa Machi 6, 2025.