Bilioni 82 kujenga daraja la pangani, kurahisisha shughuli za kibiashara

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Leo, Februari 26, 2025 aweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa daraja la Pangani ambapo ujenzi wake umetoa ajira kwa vijana wa Mkoa wa Tanga na Mikoa ya jirani.

Hatua hiyo imefikiwa na Dkt. Samia akiendelea na ziara yake ya kikazi Mkoani Tanga huku mradi huo wa ujenzi wa daraja la Pangani lenye urefu wa mita 525 limegharimu shilingi bilioni 82.

Daraja hilo litaunganisha barabara ya ushoroba pwani inayoanzia eneo la Malindi  kwenda Hororo- Bagamoyo – Tanga, ambapo linatarajia kurahisisha usafirishaji mazao ya biashara na chakula pamoja na kuchochea utalii na uchumi wa bluu na kuondoa changamoto ya wakazi wa Pangani  kutegemea kivuko MV Tanga pekee kuvuka mto Pangani.

Aidha, wakazi wa Wilaya ya Pangani wamempongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa daraja hilo pamoja na utekelezaji wa miradi mingine Wilayani humo ikiwemo miradi ya maji, shule, afya na ujenzi wa josho la mifugo kwa ajili ya jamii ya wafugaji lenye thamani ya shilingi milioni 38.