Dkt. Samia akubali ombi la kujenga ukuta wa makaburi ya msambweni Tanga

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekubali ombi la kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa Makaburi ya Masambweni ambazo ziliombwa na waumini wa Msikiti wa Ijumaa wakati akiweka Jiwe la Msingi la upanuzi wa Msikiti huo leo Februari 26, 2025.

Rais Dkt. Samia amesema “Nimelisikia ombi lenu la kuchangia ujenzi wa uzio eneo la Makaburi la Msambweni, sasa hili ni jambo la kiimani naomba nilibebe mimi mwenyewe”.

Waumini wa Msikiti wa Ijumaa wamempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujitolea kwake na kumuombea baraka ili aendelee kuliongoza vyema Taifa.