Mrembo wa Nigeria, Sophia Egbueje, ameonyesha video yake akipokea gari lake jipya la kifahari aina ya Lamborghini, hatua inayokuja baada ya kudai kuwa msanii maarufu wa Afrobeats, Burna Boy, alishindwa kutimiza ahadi aliyompa.
Siku ya jana, Sophia alivujisha sauti yake mtandaoni akielezea jinsi alivyojisikia kusalitiwa baada ya kulala na Burna Boy bila kupewa gari la kifahari aliloahidiwa. Katika sauti hiyo, alilalamika kuwa alitumaini kupata zawadi hiyo, lakini hakupata chochote kama alivyoahidiwa.
Baada ya kilio chake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, Sophia sasa ameonekana akijivunia Lamborghini mpya, ingawa haijafahamika wazi kama imenunuliwa na yeye mwenyewe au kama ni mtu mwingine aliyemnunulia.

Tukio hili limezua gumzo mitandaoni, huku mashabiki wakitoa maoni tofauti juu ya madai yake dhidi ya Burna Boy na hatua yake ya kujionyesha na gari jipya.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.