Bodi ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (IFAB) imetangaza mabadiliko kadhaa ya Sheria za Mpira wa Miguu ikiwemo kanuni itakayotumika kutoa adhabu kwa mlinda mlango atakayepoteza muda makusudi, ambayo itaanza kutumika msimu ujao wa 2025/26.
IFAB imethibitisha kuwa mabadiliko hayo ni ya sheria namba 12.2 inayohusu pigo la adhabu (Indirect free kick) ambapo, iwapo mlinda mlango hatouachia mpira ndani ya sekunde nane mwamuzi atalazimika kuipa timu pinzani pigo la kona.
Mabadiliko hayo yamefanyika kutokana na changamoto ya walinda milango kupoteza muda kwa kiasi kikubwa na kusababisha utata katika mechi mbalimbali.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.