Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba Sc, Ahmed Ally na Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga Sc, Ally Kamwe wote wameitwa kwenye Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kwa tuhuma za kutenda makosa ya kimaadili.
Wawili hao wameripoti asubuhi ya leo, Machi 3, 2025 kwenye ofisi za TFF zilizopo Karume, Dar es Salaam kwaajili ya kusikiliza kusomewa makosa yao na hukumu.
Ikumbukwe kuwa Jumamosi Machi 8, Simba na Yanga watakuwa kwenye Dimba la Benjamin Mkapa, kwenye mchezo wa Kariakoo Derby.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.