Kesi ya Ahmed, Kamwe yasogezwa mbele

Kesi ya kimaadili inayowakabili Meneja Habari, Mawasiliano wa Simba Sc, Ahmed Ally na Meneja Habari, Mawasiliano wa Yanga Sc, Ally Kamwe iliyopaswa kuzikilizwa leo Machi 3, 2025 imeharishwa hadi kesho, Machi 4, 2025 saa 6 mchana, baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kupata dharura.

Wawili hao waliripoti asubuhi ya leo, kwenye ofisi za TFF zilizopo Karume, Dar es Salaam kwaajili ya kusikiliza makosa yao na kutolewa hukumu.