Mama mjasiriamali Arusha amuunga Mkono Rais Samia kutumia nishati safi

Mama mjasiriamali, Elizabeth Majura mkazi wa Kwa Mromboo Mkoani Arusha ameonyesha shauku ya kununua mashine zinazotumia nishati safi ya kupikia kutokana na athari za kiafya anazopata kwa kutumia kuni kwenye biashara ya Bakery aliyomfungulia kijana wake wa kiume aliyekata tamaa baada ya kufeli kidato cha nne. 

Kuelekea siku ya Mwanamke Duniani, Mama huyo ameonyesha uthubutu kuwa wanawake ni Viongozi ambao wanaweza kuwainua watu wengine katika ngazi ya familia na Taifa kwa Ujumla.