Baba Wa Davido Akamilisha Mradi Wa Umeme Wa Tsh Trilioni 5.2/=

Wakazi wa Nigeria wana kila sababu ya kusherehekea baada ya bilionea Adedeji Adeleke, baba yake @Davido, kukamilisha mradi wa umeme wenye thamani ya dola bilioni 2 (Tsh Trilioni 5.2/=). Mradi Huu Utatoa umeme kwa zaidi ya watu milioni 3 kwa gharama ambayo ni nafuu zaidi kuliko Ule Wa NEPA (Shirika la Umeme la Nigeria).

Wakati Davido akiendelea kuipeperusha bendera ya Nigeria kupitia muziki wake duniani, baba yake anahakikisha wananchi wanapata maendeleo ya msingi (ajira na umeme) wa uhakika kwa bei nafuu. Hatua hii si tu kwamba itapunguza utegemezi wa umeme usio wa uhakika, bali pia itachochea ukuaji wa uchumi kwa biashara na viwanda vidogo ambavyo vimekuwa vikihangaika na changamoto za umeme wa gharama kubwa.

Mradi huu unadhihirisha jinsi familia ya Adeleke inavyowekeza katika ustawi wa Nigeria kwa nyanja tofauti; burudani na maendeleo ya miundombinu.