Spotify Yalipa Tsh Trilioni 26.5/= Kwa Wasanii Duniani.

Spotify imelipa $10B (Tsh trilioni 26.5/=) kwa wasanii duniani mwaka 2024, kiwango cha juu zaidi kuwahi kutolewa na kampuni moja ya mauzo ya muziki.

Hata hivyo, malipo haya yamezua mjadala kuhusu mgao wa mirabaha, hasa baada ya waandishi wa nyimbo walioteuliwa kwenye tuzo za Grammy mwaka Huu kugomea hafla ya Spotify wakilalamikia mapato madogo kulinganisha na usikilizaji wa kazi zao.

Msemaji wa Spotify alisema kuwa mgawanyo wa fedha hizo ni jukumu la lebo za muziki na wachapishaji, si kampuni yenyewe. Wadau wa muziki wanaendelea kudai uwazi zaidi. Fahamu Kuwa Spotify Sio Sehemu Pekee Ya mapato Kwa Wasanii, Kwani Pia Hupata Mapato kutoka vyanzo vingine kama ziara za muziki na mikataba ya biashara.