Simeone akiri Barcelona ni klabu Bora

Kocha wa Atletico De Madrid, Diego Simeone amekiri kuwa Barcelona ndiyo klabu inayocheza soka bora zaidi duniani.

“Nimewahi kusema hivyo na leo narudia tena, Barcelona ni timu inayocheza soka bora”.

“Pia ni timu inayojumuisha uchezaji bora wa timu, na ina wachezaji utakaowatofautisha katika kiwango cha mtu mmoja mmoja,” amesema Simeone.