Lionel Messi, hatashiriki katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2026 za timu yake ya taifa ya Argentina mwezi huu (Machi 2025) kutokana na jeraha la misuli alilopata hivi karibuni akiwa na klabu yake ya Inter Miami.
Katika mechi ya hivi karibuni ya Major League Soccer (MLS), Messi alifunga bao muhimu katika ushindi wa magoli 2-1 wa Inter Miami dhidi ya Atlanta United.
Hata hivyo, baada ya mchezo huo, alihisi maumivu kwenye misuli ya paja, vipimo vya MRI vilionyesha jeraha dogo kwenye misuli na kupelekea kutolewa kwake kwenye kikosi cha Argentina kitakachokabiliana na Uruguay na Brazil katika mechi zijazo za kufuzu Kombe la Dunia 2026.
Kulingana na taarifa hiyo Messi amefunguka na kusema amepatwa na huzuni kubwa kutokuwepo kwenye mechi muhimu za kuisaidia timu yake kupambana kufuzu kushiriki Kombe la Dunia 2026.
“Nina huzuni kukosa mechi hizi muhimu dhidi ya Uruguay na Brazil, nilitamani sana kucheza, lakini jeraha dogo nililopata linanigharimu kupumzika kidogo, kwa hivyo siwezi kuwa hapo”.
“Nitakuwa nikiunga mkono na kushangilia nikiwa nje ya uwanja kama shabiki mwingine yeyote,” amesema Messi.
Messi, mwenye umri wa miaka 37, atabaki Marekani kwa ajili ya matibabu na uwezo wake wa kurejea uwanjani utategemea maendeleo yake katika matibabu na jinsi atakavyoitikia programu ya kupona.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.