Tyla Ashinda Msanii Bora Wa Mwaka Wa Dunia Tuzo Za iHeart Radio Music Awards 2025

Muimbaji Wa Afrika Kusini, Tyla, ameendelea kuandika historia katika muziki wa kimataifa baada ya kushinda tuzo ya “World Artist of the Year” kwenye Tuzo Za iHeartRadio Music 2025 Zilizotolewa Usiku Wa Kuamkia Leo Huko Los Angeles, Marekani.

Hii ni mara ya kwanza kabisa tuzo hiyo kutolewa, na ushindi Wa Tyla unazidi kuthibitisha ukuaji wa muziki wa Afrika kwenye jukwaa la dunia.

Tyla Alikuwa Akiwania Tuzo Hiyo Na Wasanii Wengine Kama; YG Marley, Burna Boy, Tems Pamoja Na Rapa Wa Uingereza “Central Cee”. Washindi Wengine Wa Tuzo Hizi Ni Pamoja Na Taylot Swift, Billie Eilish, SZA, Glorilla N.k .

Kumbuka Pia 2024 Tyla Alishinda Tuzo ya Grammy kipengele cha “Best African Music Performance”.