Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, klabu ya Yanga, baada ya kutoridhishwa na majibu ya Bodi ya Ligi Kuu (TFF), imeamua kuchukua hatua ya kisheria na kufungua kesi ya malalamiko kwenye Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS). Ingawa taarifa hii bado haijathibitishwa rasmi, vyanzo mbalimbali vya habari vinadai kuwa Yanga imeamua kusonga mbele na kudai haki yao kupitia njia ya kisheria.
Yanga hawakukubaliana na majibu yaliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu na wamesema hawana imani na mwenendo wa Bodi hiyo. Katika hatua hii, wameamua kufungua kesi kwenye CAS kwa ajili ya kudai haki yao, wakilenga kurejesha hali ya ufanisi katika suala la kifungo cha alama 3 na mabao 3 ambavyo walidai kisheria.
Aidha, kwenye ukurasa wa Makamu wa Rais wa klabu ya Yanga ameanza kuonyesha post za tafsiri tofauti, ikiwemo mojawapo iliyoandikwa: “KUWA MAKINI SANA NA MAJI YALIYOTULIA,” pamoja na hashtag #NasahaZaAAH. Kisha akaandika tena “Unaweza kuendesha watu ila huwezi kuwaendesha wakati wote, unaweza kuburuza watu ila huwezi kuwaburuza wakati wote, unaweza kuwaongopea watu ila huwezi kuwaongopea wakati wote, kuwa makini na maji yaliyotulia, yana kina kirefu sana.” Maneno haya yaliandikwa na Makamu wa Rais wa klabu ya Yanga na kuungwa mkono na baadhi ya viongozi wa klabu na mashabiki wa Yanga.
Kwa sasa, malalamiko ya Yanga yako mbele ya CAS na kinachosubiriwa ni taratibu za kisheria kabla ya kesi hiyo kusikilizwa. Hata hivyo, hakuna taarifa rasmi iliyothibitisha habari hizi kutoka kwa vyanzo rasmi vya Yanga au Bodi ya Ligi Kuu.
Leave a Reply