Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali inaendelea kukamilisha ujenzi wa mradi wa uzalishaji umeme katika Bwawa la Julius Nyerere kwa gharama ya shilingi trilioni 6.6. Ujenzi wa mradi huo wenye uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 2,115 kwa siku umekamilika. Hadi Machi 2025, jumla ya megawati 2,115 zimeunganishwa kwenye gridi ya taifa na hivyo kuongeza kiwango cha umeme katika gridi ya taifa kufikia megawati 4,031.7.
Majaliwa amesema Kuanza kwa uzalishaji wa umeme katika mradi huo kumeongeza kiwango cha upatikanaji wa umeme wa uhakika na kuwa chachu ya kasi ya maendeleo ya nchi.
Majaliwa ameeleza hayo wakati anawasilisha bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2025/2026 leo Bungeni jijini Dodoma
Mradi wa JNHPP Umeongeza Upatikanaji wa Umeme wa Uhakika- Waziri Mkuu Majaliwa

Leave a Reply