Kwa Mujibu Wa Ripoti Mbalimbali, Mahakama ya Manhattan Nchini Marekani, imempa #Davido siku 21 kujibu kesi ya madai ya kuiba wimbo. Wasanii wanne kutoka Nigeria “Martins Chukwuka, Abel Umaru, Kelvin Campbell, na David Ohioghena” wanamtuhumu Davido kuiba wimbo wao Uitwao “Work” Wa 2022 na kuutumia kutengeneza Ngoma Yake Ya “Strawberry on Ice” Alioutoa 2024.
Wasanii Hao Wanadai Kuwa Walituma wimbo Huo kwa Davido kwa ajili ya collabo Januari 2022, lakini badala yake alimpa Emmerson (msanii wa Sierra Leone) Na Kisha Kuu-sample bila ruhusa. Madai yanaonyesha Davido alikubali kulipa $45,000 (Tsh Milioni 120/=) na kugawana mirabaha, lakini hakutimiza makubaliano hayo. Hivyo wasanii hao wanadai fidia ya $150,000 (Tsh Milioni 400/=) pamoja na haki zao za umiliki wa wimbo.
Wimbo wa ‘Work’ ambao unadaiwa kuwa Davido Ameu-Sample katika Ngoma Yake Ya ‘Strawberry on Ice’ bado haujapatikana Kwenye Majukwaa Ya Kusikilizwa Muziki, Kwani Hata baada ya kusambaa kwa taarifa za kesi Hii, hakuna kipande cha wimbo huo kilichowekwa kwenye Digital Platforms Za muziki kama YouTube, SoundCloud, au Apple Music. Hii inaweza kuwa wimbo huo haujatoka rasmi au Ulitumika kama demo tu Kabla ya kutokea kwa mzozo huu Au Uliwekwa Private.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.