Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Imekuwa mstari wa mbele kuendeleza michezo mbalimbali huku vilabu vikongwe (Simba na Yanga) vikinufaika na mapenzi ya dhati ya Rais Samia Kwenye michezo
Kwa upande wa Jangwani, Rais Samia alitoa fedha za kutosha Kwa Yanga na hakuishia hapo pia alitoa ndege ya Air Tanzania kuwapeleka Vijana wa Yanga na Mashabiki wake fainali nchini Algeria ya Kombe la Shirikisho, Ndege iliyowapeleka na kuwasubiri.
RAIS Samia aliwaambia wazi GSM na Wafanyabiashara kuwa hawabani bani kwenye kodi kwakuwa anataka kile kinachosalia wakakitumie haswa kwenye michezo, anataka Watanzania waneemeke na anataka klabu zetu zipige hatua, matokeo yake Yanga walicheza fainali ya Shirikisho na kufika Hatua ya robo fainali ya Klabu bingwa msimu uliofuata.
Kwa upande wa wekundu wa msimbazi Simba, baada ya misimu mingi kuishia robo fainali, sasa wapo Nusu fainali ya Shirikisho kufuatia hamasa ya bao la mama. Rais Dkt. Samia amemwaga fedha za kutosha kwenye goli la Mama, ameongeza mzigo kwenye mechi ya mwisho ya robo fainali kutoka Million tano mpaka million 10 kwa goli, ni mahaba yake kwa mchezo huu pendwa na timu zake, ni mahaba yake kutaka soka la Tanzania lipige hatua
Leave a Reply