Diamond Tajiri Kuliko Burna Boy, Wizkid Na Davido.

Mchekeshaji Kutoka Nigeria @comediandeeone Amesema Kwamba Mwanamuziki @diamondplatnumz Ni Tajiri Kuliko #BurnaBoy, #Wizkid Na #Davido Kwa Pamoja. Hii Ni Baada Ya Video Za Diamond Ku-trend Africa Zikimuonesha Alivyokuwa Anatunza Hela Kwenye Harusi Na Afterparty Ya @juma_jux & @its.priscy Huko Lagos, Nigeria .

“Sikuamini Kama Wasanii Wa East Africa Wana Pesa Kiasi Hiki Katika Maisha Yangu, Hii Sio Kelele Tu! Ni Pesa Kweli…. Kwani Amekuja Kwenye Harusi Ya Jux & Priscilla Na Kutumia Zaidi Ya Dola 350,000 (Tsh Milioni 939/=). Kwanza Kiasi Tu Ambacho Alikuwa Anatoa Kwa Kila Mtu Kwa Pamoja Ni Zaidi Ya $100K (Tsh Milioni 268/=), Alikuwa Amewapatia Hadi Polisi Dola 100, 100”

“Sio Wasanii Wa Huku Wanakuahidi Na Bado Hawakupi Kitu, Wasanii Wa Nigeria Itabidi Muwe Wapole, Kuna Pesa Upande Mwingine Wa Africa, Ebu Tazama Waafrika Mashariki Wakimwaga Cash, Sikuamini Kabisa Hii Kwa Diamond, Hata Meno Yake Ya Diamond (Almasi) Ni OG, Sio Hawa Wasanii Wetu Kutwa Kufeki Maisha Tu” – Comedian Deeone