Mkuu wa Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Jenerali Jocob John Mkunda ametangaza nafasi za kuandikishwa Jeshi la wananchi Kwa vijana wenye elimu ya Sekondari hadi elimu ya Juu.
Akizungumza leo aprili 30,2025 Makao ya Jeshi Hilo msalato Jijini Dodoma Kwa Niaba ya Mkuu huyo wa Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania Msemaji wa Jeshi hilo Kanali Gaudentius Ilonda amesema kuwa nafasi zinazoandikishwa na Jeshi hilo ni kwa vijana wenye elimu ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita umri usiozidi miaka 24, Vijana wenye elimu ya Stashahada umri usiozidi miaka 26, Vijana wenye elimu ya Juu umri usiozidi miaka 27 na Madaktari Bingwa wa
Binadamu umri usiozidi miaka 35 ya kuzaliwa.
Kanali Ilonda amesema kuwa utaratibu wa Maombi hayo yaandikwe Kwa mkono na Muda wa kuwasilishwa Maombi hayo ni kesho mai 1 ,2025 na mwisho mai 14 2025 na yaambatanishwe na nakala ya kitambulisho Cha Taifa pamoja na namba ya NIDA, nakala ya cheti Cha kuzaliwa, Cheti Cha shule, chuo na namba ya simu ambayo itakuwa rahisi Kwa mawasialiano.
Aidha Kanali Ilonda ametoa angalizo baada ya kutangaza nafasi hiyo ya kuandikishwa Jeshini ambapo amesema kuwa wananchi wasikubali kutapeliwa na matapeli Kwa kisingizio Cha kupata nafasi ya Jeshi Kwa kutoa fedha
“Nitoe angalizo Kwa wananchi Hakuna nafasi ya kuandikishwa Jeshini Kwa kutoa fedha msikubali kutapeliwa” – amesema Kanali Gaudentius Ilonda
Leave a Reply