Msanii Wa Muziki (Singeli) Nchini Kutoka Label Ya #WcbWasafi @itsdvoice 🇹🇿 ametangaza kuachia EP yake Mpya na ya kwanza Tangu Aanze Muziki, hatua inayokuja kama sehemu ya mwendelezo wa mafanikio makubwa aliyoyapata kupitia kazi zake za awali.
D Voice Amethibitisha Hilo Kupitia Ukurasa Wake Wa Instagram Kwa Kuandika; “Can’t Wait For My First EP”.
Ep Hii Itaifuata Album Yake Ya Kwanza ‘Swahili Kid’ Iliyofanya Vizuri Kwenye Majukwaa Mbalimbali Ya Kusikiliza Muziki N.k Huku Lengo Lake Kubwa Ni kuona Singeli ikisikika katika majukwaa ya kimataifa Kwa Kutumia lugha ya Kiswahili kama nyenzo ya kueneza utamaduni wa Kitanzania.
Hadi Sasa D Voice Ndio Msanii Wa Singeli Afrika Mashariki Mwenye Streams Nyingi Zaidi Kwenye Platforms Mbalimbali Za Kusikiliza Muziki (Youtube, Boomplay, Audiomack N.k).
JE, Unatamani EP Hii Mpya Ya D Voice Itoke Lini?/ Utamani Kumsikia Msanii Gani Katika EP Hii ⁉️
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.