Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia Diana Edward Bundala (42), ambaye pia hujitambulisha kama ”Mfalme Zumaridi’, mkazi wa mtaa wa Buguku, kata ya Buhongwa.
Taarifa kutoka kwa Jeshi la Polisi inasema kuwa Zumaridi anahojiwa kwa tuhuma za kuendesha shughuli za kidini bila kusajiliwa na kufanya mahubiri kwa sauti kubwa, hivyo kusababisha usumbufu kwa majirani.
Aidha, polisi wanaendelea kumhoji kuhusiana na picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinazomuonyesha akiwa na kundi la watoto wadogo wa kike na kiume, akiwaambia kuwa yeye ndiye Mungu wao mwenye uwezo wa kuwakinga na kifo.
“Uchunguzi kuhusiana na tukio hili unaendelea, na Jeshi la Polisi litashirikiana na taasisi nyingine za serikali katika uchunguzi huo,” ilisema taarifa ya polisi. “Tunaomba wananchi wenye taarifa mbalimbali zinazoweza kusaidia uchunguzi wa tuhuma hizi wazifikishe kwa Jeshi la Polisi.”
Jeshi la Polisi limeongeza kuwa mara uchunguzi utakapokamilika, hatua za kisheria zinazostahili zitachukuliwa dhidi ya mtuhumiwa.
Leave a Reply