Wizara ya Uchukuzi kupitia kwa Waziri wake Prof. Makame Mbarawa amelieleza Bunge la Tanzania leo Alhamisi Mei 15, 2025 kwamba serikali kupitia Shirika la reli Tanzania TRC Mwezi Juni, 2025 itaanza rasmi usafirishaji wa mizigo kwa kupitia Reli ya kisasa ya Standard Gauge Railway (SGR).
Prof. Mbarawa amebainisha hayo wakati akieleza kuhusu jitihada zinazochukuliwa na serikali katika kuchagiza ukuaji wa uchumi nchini, akisema Serikali pia limeendelea kuboresha huduma za uchukuzi kwa kusimamia na kuendeleza huduma na miundombinu yenye kufikia urefu wa Kilomita 2, 707 pamoja na Kujenga reli mpya ya kisasa ya SGR kwa awamu kadri ya upatikanaji wa fedha utakavyokuwa.
Serikali pia inao mpango wa ujenzi wa reli ya SGR kwa maeneo mengine ikiwemo Ujenzi wa reli ya kisasa kwenye ushoroba wa Kusini na Kaskazini ili kuhakikisha miundombinu inakuwa nyenzo kuu katika kuchagiza ukuaji wa uchumi nchini Tanzania.
Akizungumzia mafanikio ya usafiri wa treni katika reli ua SGR hadi kufikia Machi 2025, Waziri Mbarawa amebainisha kuwa Jumla ya abiria 2, 054, 828 wamesafirishwa na hivyo kuwezesha makusanyo ya mapato ya Bilioni 60.25, ikisaidia pia kupungu,a muda wa safari kutoma saa tisa zilizokuwa zinatumima kwa usafiri wa barabara hadi kufikia saa tatu kati ya Dar Es salaam na Dodoma.
“Punguzo hilo la muda limewezesha muda uliopunguzwa kutumika katika shughuli nyingine za uzalishaji mali.” Amebainisha Waziri Makame Mbarawa
Leave a Reply