Klabu ya RS Berkane ya Morocco imetwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) kwa mara ya tatu katika historia yake, baada ya kuibuka na ushindi wa jumla wa mabao 3-1 dhidi ya Simba SC ya Tanzania.
Fainali hiyo ya pili ya marudiano imechezwa katika dimba la New Amaan Complex, Zanzibar, ambapo mashabiki lukuki walijitokeza kushuhudia pambano hilo la kihistoria.
Simba SC, ambayo ilikuwa na matumaini makubwa ya kutwaa taji hilo kwa mara ya kwanza, imeshindwa kutimiza azma hiyo mbele ya Rais wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi, hali inayoibua kumbukumbu ya mwaka 1993, ambapo pia Simba ilipoteza fainali nyingine mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa wakati huo, Ali Hassan Mwinyi, ambaye ni baba wa Rais wa sasa wa Zanzibar.
Kwa ushindi huo, RS Berkane inajizolea sifa kama moja ya klabu bora za Afrika kwa upande wa mashindano ya CAF Confederation Cup, ikifikisha mataji matatu (3), baada ya yale ya miaka ya 2020 na 2022.
Leave a Reply