Usher agombana na Kevin Hart jukwaani baada ya kuvamia tamasha lake bila mualiko

Kevin Hart alishangaza watazamaji huko Inglewood, California kwenye tamasha la Usher hii ni baada ya mchekeshaji huyo kutumbuiza bila shati, akimuiga Usher na kuimba ‘Nice & Slow.’

Usher alijiunga haraka na Hart jukwaani, na kumuuliza ‘Unafanya nini?!’

Hart  kisha alitania kuhusu makubaliano ya kuimba wimbo huo, kabla ya kuondoka hatimaye akazua maneno mengi mitandaoni.

‘Katika hali ya kushangaza, Kevin Hart alipanda jukwaani wakati wa tamasha la Usher huko Inglewood, California, kiasi cha kushtua na kufurahisha watazamaji’ vyanzo vya habari vya burudani vilisema.