Diamond Amjibu Mbosso Kuhusu Babalevo.

Simba 🦁 @diamondplatnumz Amemjibu @Mbosso_ Baada Ya Kumtaka Amuonye @officialbabalevo . Diamond Kupitia Ukurasa Wake Wa Instagram (Story) Ameeleza Kuwa Hakutaka Mambo Yaende Mitandaoni Kwani Alimtafuta Mbosso Kwa Hekima Na Kumueleza Kila Kitu. Pia Amesema kuwa kila mara aliposhirikiana na Rayvanny, Mbosso alionekana kukasirika, jambo ambalo si sahihi kwa mtu anayekua kwenye tasnia.

ā€œnaona unalazimisha kuhitalifiana na mimi nikuongezee mwendo, okay wacha nikuridishe…

kwanza kabisa sikutaka mitandao, nilikupigia simu na kukutumia messages na tulipokutana niliongea na wewe kwa hekima na ushahidi namna gani nimekuwa sipendezewei na nimekuwa nikimsema baba levo anachokifanya. tena nikikuonesha kwa ushahidi na nikikuambia kuwa hakina faida kwangu zaidi ya kunitia tu ubaya!

lakini pia nilikuambia msanii anapotoka kwenye lebo usitegemee wote watakuwa na reaction za kufanana. wengine watakuwa na reaction mbalimbali, kuna wengine wanaweza wakawa wanareact vitu ambavyo sio vizuri kwa maumivu ya kukupenda tu kuona ā€œdah, ndugu yetu kwaio katoka kwenye teamā€¦ā€

nikakuambia jitaahidi kutumia busara, maana hayo ni mambo ya kawaida na unapaswa kujua binadamu wako hivyo. usipokuwa makini utaona kila mtu katumwa na diamond, then utaishia kunichukia na kugombana na mimi bila sababu…

na nikakutolea mfano hai kuwa hata wewe alipokuwa ametoka rayvanny, ulikuja nyumbani kwangu na hasira kuniambia maneno kedekede ya kumchukia rayvanny na ulipinga kabisa nisifanye nae nyimbo ya ā€œnitongozeā€ na wala nisishirikiane nae kwa lolote…

nikakuambia hapana, si vyema. mtu kutoka kwenye lebo sio uadui, ni jambo la kawaida. kuna time itafika hata wewe utapaswa pia kutoka kwenye lebo kuanza maisha ya kujitegemeaā€¦ā€œ – Diamond Platnumz