Romyjons Amjibu Lavalava Kuwa hafanyiwi fitna ila kazi zake mbovu.

Baada ya msanii @iamlavalava kudai kupitia Instagram kuwa ndiye msanii anayeongoza kufanyiwa fitna kila akitoa kazi mpya, DJ maarufu Africa kutoka Nchini #RJ @romyjons alimjibu akisema kwamba #LavaLava hafanyiwi fitna bali nyimbo zake “sio kali kivyo,” na akashauri apewe msaada wa kuandikiwa kama wasanii wenzake.

LavaLava hakusita kumjibu RJ kwa kumkumbusha kuwa ndiye alikuwa wa kwanza kumsifia kazi zake, akisema Romy anaonekana kujisahau.

JE, Ni Kweli Lavalava Anahitaji Msaada Wa Kuandikiwa Kama Wasanii Wengine ⁉️