Nkunku akubali mkataba wa miaka mitano na AC Milan

Milan, Italia 

Klabu ya AC Milan imepiga hatua kubwa katika usajili wa mshambuliaji wa Kifaransa, Christopher Nkunku, baada ya kufikia makubaliano ya mkataba wa miaka mitano na mchezaji huyo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa ni kuwa Nkunku mwenyewe ameonyesha dhamira ya kujiunga na Milan, jambo ambalo limeipa klabu hiyo ya Serie A nguvu katika mazungumzo ya uhamisho.

Mazungumzo kati ya Milan na Chelsea, klabu anayoitumikia kwa sasa, bado yanaendelea leo. 

Chelsea wanataka kuhakikisha masharti ya kifedha ya dili hilo yanakidhi maslahi yao, huku Milan wakionekana kuwa na nia thabiti ya kukamilisha uhamisho huu haraka iwezekanavyo.

Iwapo makubaliano ya mwisho yatakamilika, Nkunku ataongeza nguvu kubwa katika safu ya ushambuliaji ya AC Milan, huku akitarajiwa kuwa mmoja wa nyota muhimu katika kampeni za ndani na za kimataifa za klabu hiyo.