Grimsby yaibua mshangao kuiondoa Man United kwenye Carabao Cup

Manchester, Uingereza 

Klabu ndogo ya Grimsby Town inayoshiriki ligi daraja la nne nchini Uingereza, imeandika historia baada ya kuiondoa Manchester United kwenye michuano ya Carabao Cup.

Mchezo huo uliochezwa jana umeacha mashabiki wengi midomo wazi, kwani Manchester United waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kusonga mbele walishindwa kuhimili presha ya Grimsby Town, ambao walicheza kwa nidhamu na ushupavu mkubwa.

Mchezo ulimalizika kwa Sare ya mabao 2-2 na Grimsby kufanikiwa kutinga hatua inayofuata kwa ushindi wa mikwaju ya penati 12-11.