‘Breezy Bowl XX’ Yatajwa Kama Ziara Namba 1 Duniani Kwa Sasa.

Ziara ya Manamuziki @chrisbrownofficial ‘Breezy Bowl XX’ yatajwa kama Ziara Namba 1 Duniani kwa sasa katika mauzo ya tiketi.

Billboard imetoa orodha ya wasanii waliokuwa kinara kwenye ‘Billboard’s Monthly Top Tours Chart’ kwa mwaka 2025 Kuanzia Januari hadi sasa:

Januari & Aprili → Coldplay waliongoza Kwa Mauzo.

Februari & Machi → Shakira alishika namba 1 Kwa Mauzo.

Mei, Juni & Julai → Beyoncé Aliongoza kwa miezi mitatu mfululizo.

Agosti → Chris Brown ameibuka kinara, ambapo ziara yake imekuwa yenye mauzo na mapato makubwa zaidi kwa mwezi huo.

Kwa mujibu wa Billboard, Breezy Bowl XX ilikusanya Kiasi Cha $96.8m (TSh BILIONI 238.2/=) kwa mwezi Agosti pekee, kupitia Shows 14 Ambapo Iliuza tiketi 590,000. Hadi sasa, ziara hiyo imekusanya jumla ya $241.4m Sawa Na (TSh BILIONI 592.6/=) Ikiwa Imeingiza mashabiki zaidi ya milioni 1.7 kwenye Jumla Ya Viwanja Alivyopiga Shows.

Chris Brown Anaendelea Kuthibitisha Ufalme Wake Katika Muziki Wa RnB Na Live Shows Duniani 🔥.