Kesi Ya Drake Dhidi Ya UMG Yafutwa.

Jaji ameitupilia mbali kesi ya madai ya kashfa ambayo Drake alikuwa ameiwasilisha dhidi ya Universal Music Group (UMG) Januari Mwaka Huu 2025.

Drake alikuwa amefungua kesi hiyo akidai kwamba UMG, wametumia maroboti na mifumo mingine ya udanganyifu kuupandisha kinamba na usikilizwaji wa wimbo wa hasimu wake Kendrick ‘Not Like Us’, Lakini Pia imechangia kumharibia sifa. Alidai kwamba wimbo huo ulieneza madai ya uongo kuhusu yeye, hasa tuhuma za unyanyasaji wa watoto…. ambazo ziliharibu jina lake na kuleta chuki dhidi yake.

Mahakama imeamua maneno hayo ni sehemu ya maoni ya kisanii na si madai ya ukweli, kwa hiyo hayawezi kuchukuliwa kama kashfa kisheria. Hivyo kesi imefutwa rasmi.