Lil Durk aomba kesi yake ifutwe.

Rapa Wa Marekani Lil Durk Kupitia Timu ya mawakili wake Amewasilisha Ombi jipya kwa jaji Akitaka kesi yake ya tuhuma za kupanga mauaji ifutwe. Wanasema waendesha mashtaka wameshindwa kutoa maelezo na ushahidi wa kutosha kuthibitisha mashtaka hayo. Hii ni kwa mujibu wa Billboard na Rolling Stone.

Kumbuka Lil Durk Alikamatwa Oct 2024 kwa mashtaka ya mauaji ya kulipia (Murder-for-hire) huko Broward, Florida.
Iliripotiwa kuwa mkali huyo wa “All My Life” Kukamatwa kwake kulitokana Na washikaji wake watano wa kundi la OTF kuhusishwa na mauaji ya Saviay’a Robinson, binamu wa Rapa Quando Rondo, yaliyotokea mwaka 2022 huko Los Angeles.

Mashtaka yanaonyesha kuwa watu hao wana uhusiano na kundi la Durk, OTF, na wanahusishwa na njama za mauaji zilizopewa msaada wa kifedha na lebo hiyo ya Lil Durk.
Mauaji ya Robinson yanadhaniwa kuwa ni kulipiza kisasi kwa kifo cha rafiki wa Lil Durk “Rapa King Von”.

Ombi La Kutaka Kesi Yake Ifutwe Imepangwa Kusikilizwa Rasmi Tarehe 18 Novemba, Mwaka Huu 2025.