Rapa Nba Youngboy aingiza zaidi ya Tsh. Bilioni. 51.3/= Kwenye Ziara Yake Ya ‘MASA’.

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, rapa @nba_youngboy ameingiza zaidi ya $21 milioni (sawa na takribani Tsh bilioni 51.3/=) kupitia ziara yake kubwa ya kimataifa iitwayo “Masa” (Make America Slime Again Tour).

Ziara hiyo ilianza rasmi mnamo Septemba 1, 2025, na hadi sasa YoungBoy ameshafanikiwa kufanya show 13 kati ya 45 zilizopangwa kufanyika katika miji tofauti nchini Marekani.

Ripoti zinaeleza kuwa kila show imekuwa ikiuzwa kwa kiwango cha juu, huku tiketi zikikamilika mapema kutokana na wingi wa mashabiki wanaomfuatilia kwa ukaribu. Vyanzo vya karibu na timu yake vinaeleza kuwa mapato hayo yanatokana si tu na mauzo ya tiketi, bali pia mauzo ya bidhaa za “merch”, mikataba ya udhamini, na ushirikiano na majukwaa ya kidijitali yanayorusha matukio ya moja kwa moja.

Endapo mwenendo huu utaendelea, inatarajiwa kwamba kufikia mwisho wa ziara mwezi Desemba 2025, YoungBoy ataweza kuvuka kipato cha $60 milioni, jambo litakalomuweka miongoni mwa wasanii wachache wa kizazi chake waliowahi kufanya ziara yenye mafanikio makubwa kiasi hicho.