Candance Adai Kanye Amemtumia Taarifa Za Watu Wanaomtishia Maisha Ili Azitoe Kama Atauawa.

Mwandishi na mchambuzi wa siasa kutoka Marekani, Candace Owens, hivi karibuni katika podcast yake, amefichua kuwa Kanye West (@ye) alimtumia taarifa za siri kuhusu watu waliokuwa wakimtishia maisha, akimpa maagizo ya kuzitoa au kuzivujisha hadharani iwapo atakuwa hatarini au atauawa.

Owens amesema kuwa yote hayo yalitokea baada ya rapa huyo kutofautiana na makampuni kadhaa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, ikiwemo sakata lake la maneno ya chuki dhidi ya Wayahudi, jambo lililosababisha mgongano mkubwa wa kibiashara na kijamii.

Aidha, Owens alieleza kuwa Kanye alikuwa mkali na makini katika kuhakikisha taarifa zote zipo kwenye mikono salama, akitumia njia ya kuwarithisha wale waliomkaribia ili kuhakikisha ukweli hauchafukiwi iwapo atakumbwa na hatari. Alibainisha pia kuwa rapa huyo alimtumia kama njia ya kutunza rekodi za vitisho na ujumbe wa hatari, jambo linaloonyesha jinsi ambavyo alihofia usalama wake na uwezekano wa mashambulizi ya kifedha au kibinafsi.

Vyanzo vinasema kwamba taarifa hizi pia zinaweza kuonyesha ushawishi wa watu fulani katika sekta ya muziki na mitandao ya kijamii, na zinaweza kufichua waathiriwa au wahusika waliokuwa nyuma ya vitisho dhidi yake, jambo linaleta mjadala mkubwa katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari.