Rapa Kodak Black Kulipa Tsh. Mil. 367+ Na Matunzo Ya Mtoto Kila Mwezi.

Rapa Wa Marekani Kodak Black, ameripotiwa kuamriwa na mahakama kulipa $10K (Tsh Mil 24.5/=) kila mwezi kama matunzo ya mtoto (child support). Zaidi ya hapo ameagizwa pia kulipa $50K (Tsh Mil 122.6/=) kwa mama wa mtoto huyo ili aweze kununua gari la kumsaidia kumsafirisha mtoto pamoja na $90K (Tsh Mil 220.7/=) za gharama za mawakili (lawyer fees).

Baby Mama Wa Kodak Black.

Hivyo Jumla Ya malipo hayo ni sehemu ya majukumu yake ya kifedha kwa ajili ya malezi ya mtoto wake na fidia ya gharama zinazohusiana na kesi hiyo.

JE, Msanii Gani Bongo Anaweza Kulipa Kiasi Hicho Cha Pesa Kila Mwezi Kama Matuzo Ya Mtoto ⁉️