Wimbo Wa Ciara Na Diamond ‘Low’ Waingia Chart Za Billboard Marekani.

Wimbo @ciara na @diamondplatnumz “Low” umeingia rasmi kwenye chati kubwa za muziki Marekani, ukishika nafasi ya #37 kwenye Billboard Mainstream R&B/Hip-Hop Airplay na #49 kwenye Billboard R&B/Hip-Hop Airplay.

Hii ni hatua kubwa kwa muziki wa Tanzania, ikionyesha jinsi Diamond Platnumz anaendelea kuipeleka bendera ya Bongo Flava kimataifa.

Kupitia mafanikio haya, Diamond anaonesha uwezo wa wasanii wa Afrika Mashariki kutokea kwenye Platforms/ majukwaa makubwa duniani. Ushirikiano wake na wasanii wa kimataifa kama Ciara unafungua milango mipya kwa muziki wa Tanzania, ukiongeza thamani ya muziki wetu katika soko la kimataifa.