Chanzo Kifo cha MC Pilipili, Polisi wafunguka

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limethibitisha kutokea kwa kifo cha Emmanuel
Mathias Matebe maarufu kama MC Pilipili mkazi wa Swaswa Jijini Dodoma na Dar es Salam, ambapo Oktoba 16 2025 majira saa 03:00 mchana, marehemu alifariki katika kituo cha Afya Ilazo akiwa anapatiwa matibabu,.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imeeleza Kabla ya kufikwa na umauti majira ya 02:00 mchana, msaidizi wake Hassan Ismaili
alipigiwa simu na mtu asiyefahamika na kuomba wakutane, na baada ya muda walifika watu watatu asiowafahamu wakiwa na Mc Pilipili ndani ya gari ndogo nyeupe na walimkabidhi Mc Pilipili akiwa na hali mbaya na kuondoka,

Uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wataalamu wa Afya umebaini, Mc Pilipili alifariki dunia baada ya kushambuliwa sehemu mbalimbali za mwili wake na watu ambao bado hawajafahamika na kupelekea kifo chake

Jeshi la Polisi limesema linaendelea na upelelezi wa kuwatafuta na kuwatia nguvuni watuhumiwa ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao