ACT Wazalendo yamvua uanachama Monalisa Ndala

Chama cha ACT Wazalendo kupitia Tawi la Mafifi, kata ya Kihesa mkoani Iringa, kimemvua rasmi uanachama Monalisa Joseph Ndala kwa madai ya kushindwa kutekeleza matakwa ya Katiba ya chama hicho,

Hatua hiyo inatajwa kuhusiana na mvutano wa karibuni juu ya uteuzi wa mgombea urais, baada ya Ndala kupinga uteuzi wa Luhaga Joelson Mpina kuwa mgombea urais wa chama hicho.

Pingamizi la Ndala lilisababisha Msajili wa Vyama vya Siasa kubatilisha uteuzi wa Mpina, ingawa ACT Wazalendo sasa wamepeleka suala hilo Mahakama Kuu. Mahakama imetoa siku tano tu kwa Serikali kujibu kesi hiyo.