Adidas Rasmi Yauza Bidhaa Zote Za Yeezy Zilizosalia.

Kampuni Ya Mavazi Ya Kimichezo Pamoja Na Masuala Ya Fashion “Adidas” Imeripotiwa Kuuza Bidhaa Zake Zote Zilizosalia Za Viatu Vya Kanye West “YEEZY” Vyenye Thamani Ya Tsh Trilioni 1.2/= Ikihitimisha Uhusiano Wake Na Rapa Huyo.

“Hakuna hata jozi moja ya viatu vya Yeezy Iliyobaki,” alisema Mkuu wa Fedha wa Adidas, Harm Ohlmeyer, baada ya ripoti ya mapato ya kampuni hiyo siku ya Jana Jumatano. “Vyote vimeuzwa, na Ukurasa Huo Tayari Tumeufunga”

Kumbuka Adidas Walivunja Mkataba Na West mwishoni Mwa Mwaka 2022 Kufuatia Kauli Zake Za Chuki Dhidi Ya Wayahudi, Na Hivyo Mapema 2023 Adidas iliamua kuuza sehemu ya hisa Za Yeezy na kutoa mapato kwa mashirika ya hisani yanayopinga ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya Wayahudi. Baadae Adidas Na Ye Walifikia Makubaliano Nje Ya Mahakama Wakimaliza Mzozo Wao Wa Kisheria Na Kuamua Kuuza Bidhaa Za Yeezy Zilizobakia.