Aliyepanga Njamaa Za Kumuua Rapa Young Dolph Akabiliwa Na Mashtaka Matatu.

kesi ya mauaji ya Rapa Young Dolph mwaka 2021 imeanza rasmi kusikilizwa mahakamani huko Memphis. Waendesha mashtaka wanadai kuwa Hernandez Govan ndiye aliyepanga Njama na kuagiza Young Dolph Auawe, Lakini Hakuwepo Siku Ya Tukio/ Siku Ambayo dolph anapigwa Risasi.

Taarifa kutoka @wreg3 zinadai kwamba Hernandez Govan ndiye aliyewaongoza Cornelius Smith Jr. na Justin Johnson, ambao tayari wamehusishwa na mauaji hayo. Smith Ambaye Alikiri kwamba yeye ni mmoja wa wauaji Wa Dolph, Mapema Jumatatu Hii Alikubali Kuwa Govan ndiye aliyewaajiri yeye na Johnson, akiwaahidi malipo na hata kuwaelekeza Mahali (Location) Ambapo Young Dolph angepatikana siku hiyo.

Wakili wa Govan Alipinga Kauli Hizo Za smith Na Kudai Kuwa Ni Uwongo Kwani Amesema Hivyo “Kwasababu anataka apunguziwe adhabu.” Kabla ya ushahidi huu, Smith Pia aliwahi kusema kwamba Big Jook (marehemu kaka yake Yo Gotti) ndiye aliyetoa oda ya malipo ya $100,000 ili Young Dolph auwawe.

Govan anakabiliwa na mashtaka matatu (3); mauaji, kula njama za kupanga mauaji na jaribio la mauaji. Mwezi uliopita alikataa makubaliano ya kukiri kosa.

Picha Ya Marehemu Rapa Young Dolph

Young Dolph alipigwa risasi November 17, 2021 kutoka kununua cookies kwenye duka moja mjini Memphis Tennessee. Uchunguzi unaeleza muuaji alifika eneo la duka hilo na kushuka kwenye gari aina ya Mercedes Benz kisha kumfyatulia risasi kadhaa Dolph hadi umauti kumfika.

Via: @theshaderoom