Aliyepeperusha Bendera Ya Palestina Wakati Kendrick Lamar Akitumbuiza Kwenye Superbowl LIX Akamatwa

Unaambiwa Mmoja Kati Ya Dancers Wa Rapa Kendrick Lamar Alikamatwa Kwenye Performance Ya Superbowl LIX Baada Ya Kupeperusha Bendera Ya Palestina Kulaani Vita Dhidi Ya Gaza.

Tukio Hilo Limetokea Wakati Kendrick Akitumbuiza Wimbo Wake Wa “Tv Off” Katika Fainali Za Superbowl LIX (Halftime) Uwanja Wa Caesars Huko Mjini New Orleans, Louisiana Nchini Marekani

Hata Hivyo NFL ilitoa tamko ikieleza kuwa kitendo hicho hakikupangwa na kwamba Dancer huyo atapigwa marufuku ya maisha kushiriki katika matukio yote ya NFL.