Amanda Remix Ya Zuchu Yatajwa Billboard.

Star wa muziki kutoka Nchini @officialzuchu ameendelea kuandika historia kimataifa baada ya kutajwa na jarida maarufu la muziki Billboard kwenye orodha ya “September Reggae/Dancehall Fresh Picks of the Month”.

Billboard imeorodhesha nyimbo 10 mpya za reggae, dancehall na soca zinazotakiwa kusikilizwa, zikijumuisha majina makubwa kama Prince Swanny, Skillibeng & Vybz Kartel, Chronic Law, pamoja na Zuchu.

Zuchu ametajwa kupitia wimbo wake “Amanda (Remix)” aliomshirikisha rapa maarufu wa jamaica @spiceofficial, hatua inayompa nafasi kubwa zaidi ya kuonekana kwenye ramani ya muziki duniani.