Amorim: Yawezekana hii ndio United mbaya zaidi kwenye histori

Meneja wa Manchester United, Ruben Amorim klabu hiyo ina matatizo makubwa lakini hayatabadili mwelekeo wake kutoka kwenye mipango yake ya kimbinu licha ya kushindwa kwa mara ya 10 dhidi ya Brighton na kuwaacha klabu hiyo katika hatari ya kumaliza ligi wakiwa na rekodi mbaya.

Brighton walipata ushindi wa 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa jana Jumapili Januari 19, 2025 na sasa United sasa wamefanikiwa kukusanya alama 11 tangu Amorim ajiunge na klabu hiyo akitokea Sporting mwezi Novemba, 2024.

“Fikiria jinsi ilivyo kwa shabiki wa Manchester United. Hebu fikiria jinsi ilivyo kwangu kwamba tunapata kocha mpya ambaye anapoteza zaidi ya kocha aliyeondoka (Erik ten Hag).

“(Lakini) sitabadilika, hata iweje. Najua tunaweza kufanikiwa, lakini tunahitaji kuishi wakati huu. Kwa sababu mimi si mjinga na ninajua kwamba tunahitaji kuishi wakati huu wa sasa.

“Sisi ni timu mbaya zaidi, labda, katika historia ya Manchester United. Najua unataka vichwa vya habari, lakini nasema hivyo kwa sababu tunapaswa kukiri hilo na kubadilisha hilo,” Amorim aliiambia Sky Sports.