Ancelloti afichua sababu za Madrid kutohudhuria Ballon D’or

Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelloti amesema kuwa klabu hiyo haikuhudhuria kwenye sherehe za tuzo za Ballon D’or kwa sababu waliamini kuwa mchezaji wao, Vinicius Jr ndiye mshindi wa tuzo hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari, kuelekea kwenye mchezo wao wa mtano wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya dhidi ya Manchester City, Ancelloti amesesisitiza kuwa Rodri alipaswa kutwaa tuzo hiyo msimu uliopita.

“Kutohudhuria tuzo za Balloon D’or haikuwa jambo baya kwa sababu tulidhani Vinicius Jr alikuwa ndiye mshindi wa tuzo hiyo, sipingi kuhusu rodri kuchukua tuzo hiyo akini nadhani angeshinda mwaka jana” amesema Ancelloti.

Tuzo za Ballon D’or zilitolewa Oktoba 28, 2024 huko Ufaransa ambapo mshindi wa tuzo hiyo kubwa duniani alikuwa kiungo wa Manchester City, Rodrigo Hernández (Rodri) akifuatiwa na Vinicius Jr wa Real Madrid.