Arsenal yageukia kwa mlinzi wa Ecuador, Hincapie

Mlinzi wa kimataifa wa Ecuador, Piero Hincapié, amekubaliana na Arsenal na kufikia makubaliano ya masharti binafsi kwa ajili ya kusaini mkataba wa muda mrefu.

Ripoti zinaeleza kuwa Hincapié ameeleza wazi kuwa anaipa kipaumbele Arsenal na anachukuliwa na kocha Mikel Arteta kama usajili sahihi kwa mipango yake ya kujenga kikosi imara.

Arsenal sasa inajiandaa kuwasilisha ofa yao ya kwanza ambayo inatarajiwa kuwa mkopo wenye kipengele cha kununua kwa lazima. 

Wakati huo huo, mchezaji mwingine wa safu ya ulinzi, Jakub Kiwior, anatarajiwa kujiunga na FC Porto katika mpango unaohusiana na dili hili.

Iwapo makubaliano yatakamilika, Hincapié ataongeza nguvu kubwa katika safu ya ulinzi ya Arsenal kuelekea msimu ujao wa mashindano makubwa barani Ulaya na ndani ya England.