Asake Ajizawadia Gari Aina Ya Tesla Cybertruck Siku Yake Ya Kuzaliwa .

Msanii Wa Nigeria @asakemusic, amejizawadia gari la kifahari aina ya Tesla Cybertruck kama sehemu ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa. Hatua hii inaonyesha mafanikio makubwa aliyoyafikia katika tasnia ya muziki.

“Birthday Gift. ………..” – Ameandika Asake Kupitia Ukurasa Wake Wa Instagram Kuthibitisha Taarifa Ya Kujizawadia Gari Hilo Wakati Akitimiza Umri Wa Miaka 30.

Uamuzi wa Asake kujizawadia gari hili si tu unasisitiza upendo wake kwa magari ya kifahari, bali pia ni ishara ya kuthamini bidii yake na mafanikio yake ya kimuziki. Thamani Ya Gari Hizo Ni Kuanzia Kiasi Cha $100K (Tsh Milioni 251+) Hadi $2M (Tsh Bilioni 5+) .