Bingwa wa zamani wa Masumbwi wa UFC, Cain Velasquez amehukumiwa miaka mitano (5) jela, sababu ikiwa ni jaribio la kuua kwa risasi mwaka 2022 dhidi ya mwanaume mmoja anayedaiwa kumfanyia vitendo vya udhalilishaji wa kingono mtoto wa kiume wa bondia huyo kwa zaidi ya mara 100.
Hukumu ya bondia huyo ilitolewa mapema Juzi, Machi 24, 2025 katika mahakama ya Santa Clara iliyopo huko California, Marekani baada ya mahakama kuelezwa namna Velasquez alivyowashambulia kwa risasi kadhaa watu watatu ndani ya gari akiwemo ‘mbakaji wa watoto’ Harry Goularte (46) ambaye ndiye anayekabiliwa na kesi ya udhalilishaji kwa mtoto wa bondia huyo mwenye umri wa miaka minne (4).
Mahakama ya Santa Clara ilielezwa zaidi kwamba shambulizi la Velasquez lilikuja baada ya Goularte kuachiwa kwa dhamana dhidi ya tuhuma hizo za udhalilishaji wa kingono zilizosababisha atiwe nguvuni na alikuwa katika mchakato wa kutumikia kifungo cha nyumbani sambamba na kufungwa kifaa maalum cha ufuatiliaji.
Imeelezwa kwamba, Velasquez alimwaga risasi kadhaa katika gari la Goularte kufuatia mfukuzano uliochukua umbali wa maili 11 (kilomita 17.7).
Hata hivyo, Goularte alinusurika kujeruhiwa, huku baba yake wa kambo ambaye ndiye alikuwa akiendesha gari hilo, akijeruhiwa na risasi hizo mara mbili.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.