Barnaba Atangaza Ngoma Mpya Na Abby Chams.

Baada ya kufanikiwa kuachia hit song yake kubwa “Salama” aliyomshirikisha nyota wa Bongo Fleva, SIMBA 🦁 @diamondplatnumz, msanii mahiri na mwenye upeo mpana wa muziki, Mopao @barnabaclassic, ameendelea kuthibitisha kuwa yupo kwenye kasi ya kutoa burudani mpya kwa mashabiki wake.

Kupitia taarifa alizotoa kwenye ukurasa wake rasmi wa Instagram, Barnaba amedokeza kuhusu ujio wa wimbo mpya aliouandaa kwa kushirikiana na kipaji kipya kinachong’aa katika anga ya muziki wa Tanzania, @abigail_chams. Wimbo huo mpya unajulikana kwa jina la “Kitu”, na umeelezwa kuwa utabeba mionjo mipya ya kimuziki, mchanganyiko wa sauti za mahadhi laini na ujumbe wa kimapenzi.

Barnaba, ambaye anasifika kwa sauti yake ya kipekee na uwezo wa kuandika nyimbo zenye kugusa hisia, amewataka mashabiki wake kusubiri kwa hamu, akiahidi kuwa “Kitu” kitakuwa miongoni mwa nyimbo zitakazoendelea kutia alama katika tasnia ya muziki wa Bongo Fleva mwaka huu.

Kwa mujibu wa tangazo lake, wimbo huu utatoka rasmi kesho Jumatano usiku, na mashabiki wanatarajiwa kushuhudia uzinduzi huo kupitia majukwaa yote ya kidijitali. Kwa kauli yake, Barnaba ameashiria kuwa hii ni sehemu ya maandalizi ya kazi nyingi anazopanga kuziachia mwaka huu, akilenga kuwapa mashabiki ladha mpya na ubunifu usio na kikomo.