Beyonce Ahitimisha Ziara Yake Ya ‘Cowboy Carter’ Jana Jijini Las Vegas.

Mwanamuziki Kutoka Nchini Marekani ‘Beyonce’ amehitimisha ziara yake ya “Cowboy Carter” kwa show ya mwisho huko Las Vegas, kuashiria mwisho wa ziara yake kwenye viwanja 32 vya majiji mbalimbali Ulaya na Marekani.

Picha ya pamoja Beyonce na Watoto Wake

Mtoto wa Beyonce ‘Blue Ivy’ ambaye amekuwa kivutio kikubwa kwenye kwenye ziara hiyo amedondosha chozi wakati yeye na mama yake wakiwashukuru na kuwaaga mashabiki.

Ziara hiyo imepokelewa kwa shangwe kubwa, huku mashabiki wakimsifu Beyoncé kwa ubunifu wake wa kipekee, sauti ya kuvutia, na uwasilishaji wenye nguvu jukwaani. Cowboy Carter imeonesha utamaduni, muziki wa country uliotiwa ladha ya kisasa, na ujumbe wa kujivunia urithi wa Kiafrika, jambo lililowagusa wengi na kuifanya ziara hiyo kuwa ya kihistoria.

Beyonce Akitumbuiza Jijini Las Vegas | Cowboy Carter Tour